Dar: RC Makonda kuwasaidia wanawake waliotelekezwa na wanaume zao
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya RC, inasema Jopo la wataalamu wa Sheria, Maafisa Ustawi wa jamii na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamejipanga ipasavyo kukuhudumia na kuhakikisha mzazi mwenzio anatoa fedha za matunzo ya Mtoto.
“Ewe mwanamke huu sio wakati wa kulia wala kuteseka, serikali yako itasimama na wewe kuhakikisha unapata haki yako uliyoikosa kwa muda mrefu,” Taarifa hiyo inaeleza.
Alisema Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya tano.

Maoni
Chapisha Maoni