DOGO JANJA: WATU WALIKUWA WANAKEJELI NA KUONGEA MAMBO KIBAO NIONEKANE MIMI KIDAGAA



MSANII wa Bongo Fleva, Dogo Janja ‘Janjaro‘ ambaye ni mume wa ndoa wa muigizaji wa Filamu Bongo, Irene Uwoya, amesema wimbo wake mpya wa ‘Wayuwayu’ ni dongo maalumu kwa watu waliokuwa wakiiponda ndoa yake bila kujua undani wao ulivyo.

Janjaro amesema hayo baada watu wengi kusema vibaya ndoa ya wawili hao kuwa hawaendani kwa kila kitu;

“Watu walikuwa wanakejeli na kuongea mambo kibao ili nionekane mimi kidagaa, sina chapaa, wananitukana lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu. ‘So’ wimbo wa Wayuwayu ulikuwa ni sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya watu na wala wasiangalie tofauti zao zilizopo”, alisema Dogo Janja.

Pia, amesema “Kwenye mahusiano kitu pekee kinachozingatiwa ni upendo, kama mnapendana na kuheshimiana vitu vingine ni vya kawaida, binadamu wamekuwa na tabia ya kuhukumu vitu kwa nje lakini hawaujui vizuri undani wake, kwa hiyo ilikuwa moja ya kufikisha ujumbe na burudani pia kwa mashabiki zangu,” alimalizia Janjaro.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ufahamu ugonjwa wa Ngiri ( Hernia) kiundani zaidi

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI