MGOGORO BAINA YA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC DHIDI YA WANANCHI WAPATIWA UFUMBUZI
MOSHI.
WAZIRI wa maji na Umwagiliaji Mhandisi,
Isack Kamwelwe amepata mwarubaini wa changamoto ya
mgogoro wa maji baina ya Mwekezaji wa kiwanda cha sukari
cha TPC na wakulima wa maeneo hayo baada ya kukaa na kufanya
mazungunzo na pande zote mbili.
Waziri huyo alisema baada ya mazungunzo na pande
hizo mbili alibaini chanzo cha mgogoro huo ni maji
ambayo hayatoshi kutokana na mabadiliko ya tabia ya
nchi na kusema serikali imeona ipo haja ya kuchimba visima vikubwa
na kujenga mabwawa makubwa ya kuifadhi maji nyakati za mvua ili
kunusuru mgogoro huo.
Ziara hiyo iliyifanyika jana ambapo
Waziri huyo alifika katika kiwanda cha Tpc ikiwa na lengo la
kutimiza agizo la Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli lililomtaka waziri huyo kuhakikisha ametatua mgogoro huo
ndani ya siku 7, alilolitoa katika kikao cha wafanyabiasha kilichofanyika Ikulu
Jijini Dar es salam mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Nimekaa na pande zote
mbili nimewasikiliza na kubaini ya kuwa maji ya umwagiliaji
yanayotumika na wakulima wa Ongama na Mwekezaji wa
TPC hayatoshi kutokana na wakulima kulima kwa
kiwango kikubwa na mabadiliko ya tabia nchi… hivyo serikali
imeona usuluwishi wa kudumu ni kuhakikisha tunashirikiana na mwekezaji kwa
kuchimba visima vikubwa,”alisema na kuendelea kuwa.
“Sanyari na kuchimba visima hivyo virefu pia
kujenga bwawa kubwa katika maeneo ya Miwaleni kata ya Kahe
Wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kutokana na kubaini eneo lile ni
tambarare na maji mengi hupote bure wakati wa mafuriko hivyo
yanaweza yakawasaidia wakulima wakati wa kiangazi,” alisema Waziri.
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI ISACK KAMWELWE.
Aidha Waziri
huyo alitoa siku sita kwa Ofisi ya
Bonde la Mto Pangani kuwasilisha idadi ya wakulima walioko katika mradi wa
umwagiliaji na kiasi cha maji kinachohitajika ili kuona namna ya
kutatua tatizo hilo kwa urahis zaidi.
“Sisi kama serikali
tunapongeza wakulima waliowekeza kwa kulima mashamba makubwa kutoka
Hekta 300 hadi wanakaribia Hekta 2000 ikiwa wanatekeleza
Serikali ya viwanda lakini pia tunampongeza mwekezaji kwa kusaidia kwa
asilimia kubwa mapato ya nchi hivyo wote ni muhimu kwetu …. bonde
hakikisheni mnaleta taarifa hiyo mapema iwezekanavyo ili kutatua changamoto
hiyo,”alisema Waziri.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa
Utawala wa kiwanda cha Sukari cha TPC, Jaffary Ally alikiri
kuwepo kwa mgogoro huo kwa zaidi ya miaka 10 sasa na kusema wapo tayari
kushirikiana na serikali kuchimba visima hivyo ambavyo
vitasaidia kumalizaka kwa mgogoro huo.
AFISA MTENDAJI WA UTAWALA WA KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC, JAFFARY ALLY.
Alisema kwa Mujibu wa kipima
maji kiwanda cha TPC kinahitajika kutumia lita 1700 kwa
sekunde huku wakulima wakihitajika kutumia lita 900 kwa
sekunde ambapo hadi kufikia sasa TPC hutumia maji lita 1000 tu kwa
sekunde kutokana na wakulima kuongezeka mashamba kutoka
hekta 300 hati hekta takribani 900.
Naye mkuu wa wilaya ya Moshi , Kippi Warioba
alisema changamoto za mgogoro huo zipo na yeye kama msimamizi wa
ulinzi na usalama kwenye wilaya hiyo atahakikisha uharibifu wa
miundombinu haufanyiki.
Aidha Afisa mtendaji wa Kata ya Tpc Arusha Chini,
Jane Mandara, alikiri kuwepo kwa changamoto ya maji hali
inayopelekea migogoro baina ya mwekezaji na wakulima.
“Tunaiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuchimba
maji ya chini ili kuweza kusaidia kupata kila mmoja haki za maji na
kuweza kuendelea na shughuli za uzalishaji,”alisema Mtendaji Jane.
Mwisho


Maoni
Chapisha Maoni