MUWSA YAJIDHATITI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

 
MOSHI.

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Moshi(MUWSA) imetenga vyanzo vitatu vya maji ambavyo vinauwezo wa kuzalisha mita za ujazo  12000 kwa siku ambapo maji hayo yanategemewa kuhudumia shughuli za matumizi ya viwanda.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka hiyo Joyce Msiru alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na jinsi mamlaka hiyo ilivyojipanga kuhakikisha viwanda vinapata huduma ya maji muda wote.

MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA), JOYCE MSIRU.
 
Alisema kuwa, mamlaka hiyo tayari imeshavitenga vyanzo hivyo vitatu na kwa sasa wameshapata vibali vya kuvitumia.

Msiru alidai kuwa vyanzo hivyo vitatu vinapatikana ndani ya mto Kikavu ambapo vitasaidia kuongeza upatikanaji wa maji katika maeneo ya viwanda.

"Mamlaka imeweka mikakati mbalimbali wakati tunaelekea kwenye nchi ya viwanda  hivyo kutakuwa na tawi maalumu ambalo litakuwa mahususi kwa ajili ya viwanda pekee yake," alisema.

Alisema kuwa mamlaka imefikia malengo ya 2020/25 ambayo yalitaka upatikana wa maji kwa mji wa Moshi uwe ni kwa asilimia 100 ambayo imeshafikiwa na mamlaka hiyo kwa sasa.

Akizungumzia suala wadaiwa sugu wa ankra za maji Msiru alisema kuwa tayari wameshafanya mazugumzo na taasisi hizo ambazo zinadaiwa.

"Ni kweli taasisi za serikali ikiwemo, Gereza kuu la Karanga, ofisi ya RPC na shule ya polisi Moshi, tunawadai lakini tumeshaanza kufikia hatua nzuri ya kufikia muafaka," alisema.

AFISA UHUSIANO WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA),RASHIDI NACHAN.
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Michael Mwandenzi,alisema upatikanaji wa maji safi na usafi Manispaa ni kwa asilimia  99.

"Wanachi  wa manispaa ya Moshi wanapata maji safi na salama kwa asilimia zaidi ya aslimia 99 hakuna mwananchi wa moshi anayefuata maji kwa zaidi ya kilometa moja," alisema

Mwandenzi alisema kuwa miongoni mwa vigezo vinavyoangaliwa kwenye tuzo za usafi ni pamoja upatikanaji wa maji safi na salama na kwamba maji Moshi yapo kwenye viwango vya ubora wa kimataifa.

Mwisho....

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ufahamu ugonjwa wa Ngiri ( Hernia) kiundani zaidi

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI