MUWSA YAKABIDHIWA MITI 7000…..
MOSHI.
MRADI wa Trees’ 4 Kili umetoa msaada wa miti 7000 kwa
Mamalaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi kwa ajili ya kupanda katika
vyanzo vya maji ili kukabiliana na upungufu wa maji na athari za mazingira na
kijamii mjini Moshi.
Mkurugenzi wa mradi wa Tree’4 Kili Thomas Munuo
amesema hayo jana katika zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha maji cha
Kaloleni kilichopo mjini Moshi na kuongeza kuwa mradi huo unakusudia kupanda
miti zaidi ya milioni Moja mwaka huu.
Amesema wanakusudia kutoa bure miche ya miti ya miti
kwa taasisi binafsi, serikali zikiwemo Hospitali,vyuo ,shule za sekondari na
msingi,makanisa na misikiti na kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu.
Munuo alisema mradi wa Trees 4 Kili umeamua kutoa
msadaa wa miche ya miti kwa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini hapa
(MUWSA) na klabu ya Moshi ili kutunzamazingira na vyanzo vya maji.
Amesema mradi wa Trees 4 Kili unakusudia kupanda miti
zaidi ya Milioni hamsini mkoani Kilimanjaro ili kukabiliana na athari za
mazingira na kijamii mkoani Kilimanjaro kwani kupungua kwa theluji na
mvua,kuongezeka kwa joto vinachangiwa na zoezi la ukataji miti ovyo.
Munuo alisema mradi wa Trees’4 kili umeanzishwa mkoani
Kilimanjaro kwa lengo la kukabiliana na athari za mazingira na kijamii na
kushukuru kampuni ya bia nchini (TBL) kusaidia mpango wa kukusanya fedha
kwa ajili ya zoezi la upandaji miche ya miti 100,000.
Mkurugenzi wa Maji safi na maji
taka (MUWSA) Joyce Msiru alisema Mamlaka yake inakusudia kupanda miche ya miti
zaidi ya 12,000 kwa mwaka huu katika vyanzo vya maji vilivyopo mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi
Warioba akiendesha zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha maji cha
kaloleni alitoa wito kwa wananchi kuuunga mkono jitihada za serikali katika
kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira kwa kuacha kufanya shughuli za
kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Mkuu huyo wa wilaya alisema ni
marufuku kwa mtu yoyote kujenga nyumba za makazi na kulima karibu na vyanzo vya
maji kwani sheria zinazuia kufanya shughuli za kipinadamu ndani ya mita sitini
kutoka katika vyanzo vya maji na kwamba serikali haita sita kumchukulia sheria
mwananchi yoyote atakayekiuka sheria hiyo.
Mwisho…
Maoni
Chapisha Maoni