VIJANA WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA
MOSHI.
UMOJA wa vijana
ya chama Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa kilimanjaro umewataka vijana kuwekeza kwenye
uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Abdulrahimu Hamad,wakati
akizungumza na umoja wa vijana wilaya wa Moshi vijijini ikiwa ni mwendelezo wa
ziara ya viongozi was vijana mkoa kutembelea wilaya zote za mkoa huo na
kukutana na Wajumbe wa mabaraza ya wilaya.
Alisema kuwa
vijana wanapaswa kuchangamikia fursa za kuwekeza katika uchumi wa viwanda kwa
kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
"Tunakiwa
kuwa kioo katika jamii kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo pia kusimamia
shughuli mbalimbali za kiuchumi,sisi wenyewe tunatakiwa tupate maendeleo
kwanza,ili jamii inayotuzunguka waone faida ya kuwa ndani ya ccm,"
alisema.
"Vijana
wanakiwa kuwa chemchemi za fikra ndani ya ccm,kwa kushiriki kikamilifu katika
kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii," alisema.
Mwenyekiti wa
UVCCM mkoa wa Kilimanjaro,Ivan Mushi ,alisema ukosefu wa ajira kwa vijana iwe
fursa ya kubuni ajira mpya kwa vijana .
"Tuitumie
changamoto ya huhaba wa ajira kama fursa za kubuni ajira na kujikwamua
kiuchumi," alisema.
Alisema kuwa zipo
njia nyingi za kujiajiri ikiwemo uwekezaji katika kilimo ,kutafuta tenda za
ujenzi wa miradi mbalimbali.
"Nitatenga
muda wakufanya ziara katika wilaya moshi vijijini ,na nitahakikisha
kushirikiana kutatua kero za vijana," alisema.
Mwenyekiti UVCCM
wilaya Moshi Hassan Husein alisema kuwa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya haina
fedha za kuendesha shughuli hali inayowapelekea kushindwa kutekeleza
majukumu mengine za kiutendaji.
Katika ziara hiyo
yenye ujumbe wa "Yajayo yanafurahisha upo tayari?" Wameongozana na
Mjumbe wa Baraza kuu la vijana Taifa, kupitia mkoa wa Kilimanjaro Nice Munissi,
Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa, Said Mndeme, Katibu hamasa na chipukizi mkoa wa
Kilimanjaro, Dickson Tarimo.
Mwisho...
Maoni
Chapisha Maoni