WANANCHI WA WILAYA YA SAME WAKUMBUSHWA KUSHIKA LESEN ZA MADINI ILI KUNUFAIKA NA GYPSUM..
Mkuu wa wilaya ya Same mkoa Kilimanjaro, Rosemary Senyamule (wa tatu kushoto) akishirikiana na Wananchi wa kata ya Bendera wilayani Same kufeka barabara jana wakati alipofanya ziara katika kata hiyo kusikiliza kero za wananchi.
SAME
MKUU
wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Senyamule amewakumbusha wananchi
wa wilaya hiyo kushika leseni za madini na kuanza kuchimba Gypsum kutoka na
kubainika kuwa Gypsum inayopatika Same inaubora mkubwa kuliko maeneo mengine.
Senyamule
alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kata ya Bendera ikiwa ni mwendelezo wa kusikiliza kero za wananchi katika
wilaya hiyo ambapo alisema kuwa imebainika Gypsum inayopatikana wilaya ya Same
inaubora mkubwa.
Alisema
kuwa, Wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa kuanza kuomba leseni za madini
zitakazowaruhusu kuchimba Gypsum na kuondokana na tatizo la ajili ambalo
limekuwa tatizo kwa vijana wengi.
“Tunatambua
kuwa vijana wamekuwa wakilalamika kwa kukosa ajira sasa vijana wa same neema
imekuja hivyo tunapaswa kuichangamkia kwa kuomba leseni ya madini na kuanza
kunufaika na uchimbaji wa Gypsum” alisema Senyamule.
Aidha
mkuu huyo wa wilaya aliuagiza uongozi wa kata hiyo kushirikiana kwa pamoja
kutenga eneo lenye madini hayo kwa ajili ya vijana hali itakayopunguza tatizo
la ajira.
Senyamule
alisema kuwa, atakaa na idara ya madini ili waweze kwenda kuwapa elimu wananchi
juu ya taratibu za kupata leseni za uchimbaji lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa
hawacheleweshwi katika kupata leseni hiyo.
Mkuu
huyo wa wilaya alisikitishwa na tatizo la mgao wa maji ya Umwagiliaji ambalo
lililalamikiwa na wananchi wa kata hiyo, na kutoa maagizo kwa wataalamu kumpa
majibu ndani ya wiki mbili kuhusiana na mgao huo huku akiwataka kuhakikisha
wanamaliza tatizo hilo ili wananchi waendelee na shughuli za kujipatia kipato.
Katika
hatua nyingine alisikitishwa kusikia lipo tatizo la Wanafunzi kubakwa ambalo
lilimkera na mara baada ya kutajiwa mtu anayehusika kuwafanyia wanafunzi
kitendo hicho aliamuru jeshi la Polisi kumkamata na kumfungulia kesi haraka
huku pia akiondoka na wanafunzi wa kike wapatao wanne waliofanyiwa kitendo
hicho cha ukatili.
Pia
aliwaasa viongozi wa kata kutowachelewesha wananchi kwenye maendeleo na badala
yake washirikiane kwa pamoja bila kujali itikadi ya vyama kwani maendeleo
hayana chama.
Katika
ziara hiyo ambayo mkuu huyo wa wilaya aliongozana na wataalama mbalimbali toka
halmashauri walishirikiana na wananchi kufanya usafi katika barabara.
Mwisho………..

Maoni
Chapisha Maoni