UVCCM KILIMANJARO:Maalim Seif Ujiuzulu siasa umechoka

KILIMANJARO.

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa Kilimanjaro  umesema siasa za maji taka, uongo fitna na majungu, zimepitwa na wakati hivyo umemtaka Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akubali kiungwana kujiuzulu siasa na kupumzika.

Umeeleza kuwa Mwanasiasa huyo hadi leo kubaki kwenye ulingo wa siasa wakati wenzake wengi wameachia ngazi ,yaonyesha ana ajenda ya siri ambayo mtu mwingine ndani ya CUF hana siri hiyo .

Matamshi hayo yametamkwa jana na Katibu  wa UVCCM Mkoa Kilimanjaro Abdulrahim Hamid  alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tuhuma dhidi ya Makamo wa Rais Mama Samia zilizotolewa na Maalim Seif hivi karibu wakati akiwa mkoa Kusini Unguja .

Hamid alisema kama yupo mwanasiasa mwenye vyama viwili Zanzibar hawezi kuwa mbele ya Maalim Seif kwani ndiye mwanasiasa mwenye vigezo vyote vya kuwa na imani ya kisiasa na kadi mbili kwa wakati mmoja .

Alisema si jambo la kawaida kama kweli Maalim Seif si rafiki wa serikali za CCM aweze kuingia kwenye vikao mazungumzo muhimu akikabiliana na viongozi  saba  wa CCM na yeye akiwa peke yake bila kusindkiizwa na Kiongozi toka chama chake.

"Anafahamika kitambo Maalim Seif  ni bingwa1 wa siasa za maji taka na kuchongea wenzake tokea enzi za Marehemu Aboud Jumbe. Kwa  bahati mbaya sana siasa hizo sasa zimepitwa na wakati .Kudanganya kama mama Samia ni CUF ni zaidi ya utoto kwake  "Alisema Hamid  .

Alisema kuwa haiwezekani mwanasiasa tokea enzi za kina Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Kulius Nyerere ,hayati sheikh Aboud Jumbe, Mzee Thabiti Kombo, Mzee Rashid Kawawa na wingine awe anayeshiriki  siasa hadi katika kizazi hiki(chetu).

Katibu huyo wa Mkoa alisema.
katika uzushi wake wa mwisho kwenye historia yake ya kisiasa , Maalim Seif ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kudai kuws Makamo wa Rais Samia ni mfuasi wa CUF kwani hayupo mtu atakayeamini wala kuutia akilini mwake uzushi huo.

"Maalim Seif nadhani si kwamba amechoka kifikra ,amedhoofika kisiasa .Ni busara kwake kupumzika kama wenzake kina Mzee Ali Hassan Mwinyi, Dk Jakaya Kikwete ,Waziri Mkuu Mstaafu Dk Salim Ahmed Salim,Jaji Joseph Warioba na Mzee John Malecela na Mzee Cleopa Msuya "Alisema katibu huyo wa mkoa.

Hata hivyo alisema huenda mwanasiasa huyo ana siri nzito na kiapo cha utiifu kwa waliompa maelekezo hivyo hawezi kuacha siasa hadi watimize ahadi hiyo ambayo huenda ni kulivuruga Taifa na kuwahasimisha wananchi.

"Samia kama ni mpinzani basi hakuna maana ya mtu mwingine kujiita ni mwana CCM asili kwani uana CCM wake si wa kubahatisha au wa kupigwa ramli kujua kipimo cha usafi au uzalendo alinao na uaminifu kwa chama chake "Alisema Hamid .

Mwisho..

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ufahamu ugonjwa wa Ngiri ( Hernia) kiundani zaidi

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI