Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2018

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Picha
                                                              SIHA MWENYEKITI WA WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI  (UVCCM) WILAYA YA SIHA WILSON MUSHI UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameanza kampeni maalum ya kugawa taulo za kike katika shule za msingi na sekondari wilayani humo yenye lengo la kuhakikisha wananfunzi wa kike waliofikia katika umri wa kuvunja ungo wanashiriki masomo katika kipindi chote wanapofikia katika siku zao za hedhi. Kampeni hiyo iliyozinduliwa jana na Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Siha, Wilson Mushi alisema kuwa, katika utafiti uliofanywa mwaka 2014 wilayani humo kulibainika kuwa asilimia 82 ya wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo pindi wanapokuwa katika si...