RC ATAKA MGAWANYO SAWA WA WALIMU KWA KILA WILAYA

                                                           MOSHI.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, DK. ANNE MGHWIRA (NA NNE KULIA WALIOKAA), KULIA KWAKE NI KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MKOA, DIGNA NYAKI PAMOJA NA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO OMARY MCHOME WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WA ELIMU WAKATI WA KIKAO CHA KUPOKEA TAARIFA YA MRADI WA UBORESHAJI ELIMU KWA MPANGO WA MWALIMU MAHIRI (QUALITY EDUCATION THROUGH EXPERT TEACHER SYSTEM (QUEETS).


MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anne Mghwira amewataka maafisa Elimu mkoa kwa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanafanya mgawanyo sawa wa walimu katika kila wilaya kwani wilaya za Mwanga na Same zinaupungufu mkubwa wa walimu tofauti na wilaya nyingine za Kilimanajro.

Dk. Mghwira alitoa kauli hiyo jana, katika kikao cha wadau mbalimbali wa Elimu kilichokuwa kikipokea taarifa ya Mradi wa uboreshaji wa Elimu kwa mpango wa Mwalimu mahiri (Queets), ambapo alisema kuwa zipo shule katika wilaya ya Mwanga na Same zinawalimu wawili paka watatu huku katika wilaya ya Hai na Siha kukiwa na idadi kubwa ya walimu.

Alisema kuwa, idadi hiyo ndogo ya walimu katika baadhi ya shule wilayani Mwanga na Same imekuwa ikichangia wanafunzi kufanya vibaya hali ambayo imepelekea kwa sasa wazazi kuanza kulalamikia tatizo hilo la uchache wa walimu.

“Maafisa Elimu mkoa mnapaswa kuangilia tatizo hilo la uhaba wa walimu katika wilaya ya Mwanga na Same na kulitafutia ufumbuzi haiwezekani wilaya ya Hai na Siha zina na walimu wengi alafu zipo walaya ambazo hazina walimu ifike mahali sasa muone umuhimu wakuwahamisha walimu wengine kwenda kwenye hizo wilaya zenye upungufu” alisema Dk. Mghwira.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, Mradi huo wa Queets ambao katika mkoa wa Kilimanjaro unatoa huduma katika Halmashauri tatu za Moshi vijijini, Moshi manspaa na Hai, umekuwa na changamoto kubwa ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wafadhili wa mradi huo kuona umuhimu wa kufikia katika halmashauri zote za mkoa wa Kilimanjaro ili kuwasaidia walimu kujifunza mbinu na ujuzi wa kuwafundisha wanafunzi ili kuufanya mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kuwa kinara katika Elimu.

Aidha Dk. Mghwira aliwataka Walimu kuisaidia jamii kurudi katika ualisia wa Uafrika na tamaduni zake na kuacha tabia ya kuiga tamaduni zinazopotosha na kuharibu ualisia wa Muafrika.

Kwa upande wake, Meneja wa mradi wa Queets, Donatian Marusu alisema kuwa mradi huo unafadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Helvetas Swiss Inter-cooperation (HELVETAS), ambapo hujishughulisha na maswala ya Elimu na Kilimo.

Marusu alisema kuwa, kutokana na tafiti mbalimbali za elimu hapa nchini ikiwamo ya UNESCO ya mwaka 2010, ilibainika kuwa kuendelea kushuka kwa kiwango cha elimu ya msingi kumechangiwa na kukosekana kwa mafunzo ya uhakika kwa Walimu kazini.

Alisema kuwa shirika la Helvetas kwa kushirikiana na chama cha Walimu Tanzania (CWT), waliamua kuanzisha mradi wa Queets kwa kutoa mafunzo kwa walimu kwa masomo ya Hisabati, Lugha ya Kiingereza na elimu ya Sayansi ya mazingira katika wilaya za Hai na Moshi kwa mkoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

“Hadi kufikia mwaka 2017 walimu bobezi wapatao 6,612 kutoka katika shule 1800 za mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wamefundishwa kwenye mbinu na rahisi za ufundishaji pamoja na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia zinazotokana na mazingira wanayoishi” alisema Marusu.

Aidha Meneja mradi huo alibainisha kuwa, jumla ya Walimu wakuu wa shule za msingi wapatao 1,438 na maafisa Elimu kata 266 wameoatiwa mafunzo ya usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huo wa Queets.

Alisema kuwa, wanafunzi wapatao 718,000 kutoka katika shule za mradi wameweza kufaika na mardi huo kupitia walimu wao walionufaika na elimu hiyo, huku pia shule hizo zimegawiwa jumla ya vitabu vya ziada 10,627 vya masomo ya Hisabati, Kiingereza na Sayansi ya mazingira.

Marusu alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na baadhi ya walimu kutofikisha maarifa na ujuzi waliopata kwa walimu wenzao, pia kumekuwa na ufuatiliaji hafifu kutoka halmashauri ili kuhakikisha kuwa walimu wanatekeleza majukumu waliyopewa wakati wa mafunzo.

Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ufahamu ugonjwa wa Ngiri ( Hernia) kiundani zaidi

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI