WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA SIASA CHAFU
MOSHI. MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MAWENZI, MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA KILIMANJARO, DAUDI MRINDOKO (katikati), AKIWA NA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA MAWENZI CHRISTINE SHIRIMA (kushoto), NA KULIA NI MWENYEKITI WA BODI YA SHULE HIYO PROFESA CHAMBO. WAHITIMU wa kidato cha sita mwaka 2018, nchini wameshauriwa kuacha tabia ya kufanya siasa chafu pamoja na biashara haramu ya madawa ya kulevya na badala yake watumie elimu waliyoipata katika kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, Daudi Mrindoko katika mahafali ya 26 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Mawenzi iliyopo manisp...