Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

Kenya kuweka rekodi kombe la Dunia

Picha
Aden Marwa ni miongoni mwa waamuzi wasaidizi 10 kutoka Afrika watakaosimamia mechi za kombe la dunia. Mwamuzi huyo mwenye uzoefu wa miaka 7 akifanya kazi na shirika la FIFA,alifanikiwa kuorodheshwa kwenye orodha ya mwisho kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Hata hivyo hakufanikiwa kusimamia mechi yeyote. FIFA imechagua maafisa 6 kutoka barani Afrika kusimamia mechi za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi. Pamoja na hao waamuzi wasaidizi 10 wametoka barani Afrika, kwa ujumla maafisa 99 wamechaguliawa kusimamia michuano hiyo. Aden Marwa ana uzoefu wa kuwa mwamuzi msaidizi katika michuano ya kombe la dunia la vilabu 2016 nchini Japan. Alitajwa kuwa mwamuzi msaidizi wa CAF katika shirikisho la kombe la FIFA 2017 na alishiriki pia mwaka 2012,2013, na 2015 kwenye kombe la mataifa ya Afrika pamoja , kombe la dunia la walio chini ya miaka 17 , michuano ya CAF ya chini ya miaka 23 na kombe la dunia la vilabu la FIFA

Mama ajifungua mapacha wenye baba tofauti

Picha
  Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha. Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA. Hatahivyo matokea ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao. Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo. Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu.

Yajue Madhara ya kutumia Simu ya Smartphone kwenye Giza

Picha
    Mara nyingi watu wengi tuanpenda kutumia simu mahali ambapo pana giza kwa muda mrefu, sisi tunapenda kukuita kukuchati. Kuchati huku nyakati za giza wakati taa imezimwa huwa na madhara yafuatayo. Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani. Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa. Hii ni kwasababu wakati wa kutimia simu mahali penye giza huwa tunayalazimisha macho yetu yaweze kuona ya uwezo wake. Na ndo maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida. Pia utumiaji wa simu kwenye giza ...

TRA YAINGIZA MILIONI 368.77 KUTOKANA NA BIDHAA ZA MAGENDO ..

MOSHI. MAMLAKA ya Mapato nchini TRA, mkoa wa Kilimanjaro imekusanya kiasi cha shilingi milioni 368.77 kama kodi na faini za bidhaa mbalimbali zilizoingizwa nchini kinyume na sheria katika kipindi cha Julai mwaka jana hadi Februari mwaka huu. Hayo yalibainishwa na Meneja msaidi wa mamalaka hiyo mkoa wa Kilimanjaro anayeshughulikia maswala ya forodha, Godfrey Kitundu wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kudai kuwa, wapo baadhi ya Wananchi ambao sio waaminifu wamekuwa wakiingiza nchini bidhaa za magendo. Kitundu alisema kuwa, Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitumia njia zisizo rasmi (njia za panya), kupitisha bidhaa hizo ambapo katika mkoa wa Kilimanjaro zipo njia zisizo rasmi zipatazo zaidi ya 300. Alisema kuwa, mkoa wa Kilimanjaro unapakana na nchi jirani ya Kenya ambapo unanjia halali tatu zilizohidhinishwa na Serikali ambazo ni Holili, Tarakea na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambazo ndizo njia zilizopendekezwa na Serik...

VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA JUMUIYA ZAKE WATAKIWA KUACHA KULALAMIKA NA BADALA YAKE WASHIRIKIANE KUTATUA KERO ZA WANANCHI…..

Picha
MOSHI. MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani Kilimanjaro Daudi Mrindoko amewataka viongozi wa chama na jumuiya kuanzia ngazi ya kata kuacha tabia ya kulalamika na badala yake wajitoe kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi matatizo yanayowakabili Wananchi ili waendelee kukiamini chama. Mrindoko alitoa kauli hiyo jana wakati wa maadhimisho ya wiki la juma la wazazi wilaya ya Moshi mjini ambapo walipanda miti zaidi ya 200 katika shule ya Sekondari ya Kibo inayomilikiwa na Jumuiya hiyo. MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM MKOA WA KILIMANJARO, DAUDI MRINDOKO. Alisema kuwa, wapo baadhi ya viongozi wamekuwa na tabia ya kujenga lawama kwa viongozi wa juu bila kutambua kuwa hata wao wanajukumu la kuhakikisha wanashirikiana kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili Wananchi. “Wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwabebesha mizigo na lawama viongozi wa juu wakati misingi ya chama chetu ni kushirikiana viongozi wote kuhakikisha tunawatumikia ...

Yajue Madhara ya Unywaji Soda kwa Wingi

Picha
Je mwenzangu unapenda kunywa soda ngapi kwa siku? Usinipe majibu! Miongoni kati vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi mara kwa mara ni pamoja na soda ni kwa sababu wafanyabiashara mbalimbali wa vinywaji hivi pamoja na matangazo mengi ya biashara  hutangaza kinywaji hivi aina ya soda  vinywaji ambavyo hakina madhara kabisa kwa watumiaji wake. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii. Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kwa sababu maneno yangu sio sheria, lakini ni lazima ukweli nikwambie juu ya vinywaji hivi. Watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya mara baada ya kunywa soda. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe pamoja na sigara, hata kwa w...

Linda afya ya Moyo kwa kufanya hivi

Picha
Miongoni mwa magonjwa ambayo husumbua watu wengi kwa kiwango kikubwa ni moyo, hivyo ili kuweza kulinda afya ya moyo wako ili usipate magonjwa hayo ya moyo unatakiwa kufanya yafuatayo; Pima shinikizo la damu angalau mara moja kwa mwaka. Hakikisha unakuwa na uzito  sahihi. Fanya mazoezi walau nusu saa kwa siku. Punguza matumizi ya chumvi  kwenye chakula. Hapa tunanzungumzia chumvi ya mezani ambayo huongezwa kwenye vyakula kama vile nyama choma, chipsi n.k Kila wakati hakikisha unakula zaidi  matunda,mboga za majani na vyakula ambavyo havina  mafuta. Punguza matumizi na unjwaji wa pombe. Iwapo umegundulika kuwa na tatizo la shinikizo la damu,tumia dawa kama ulivyoelekezwa na watalamubwa afya na si vinginevyo.

Ufahamu ugonjwa wa Ngiri ( Hernia) kiundani zaidi

Picha
    Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni). Lakini kumbuka ya kwamba tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu ku...

Jibu la serikali kwa Maaskofu Tanzania

Picha
  Wakati wa waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini Tanzania. Rais Magufuli amewaomba wahubiri na maaskofu wazungumzie ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi. Amesema hayo akiwa katika halfa fupi jijini Dar es salaam ya ugawaji wa magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini. Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosomwa jana katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Utekwaji wa watu wa hivi karibuni, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni ba...