Machapisho

RC ATAKA MGAWANYO SAWA WA WALIMU KWA KILA WILAYA

Picha
                                                             MOSHI . MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, DK. ANNE MGHWIRA (NA NNE KULIA WALIOKAA), KULIA KWAKE NI KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MKOA, DIGNA NYAKI PAMOJA NA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO OMARY MCHOME WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WA ELIMU WAKATI WA KIKAO CHA KUPOKEA TAARIFA YA MRADI WA UBORESHAJI ELIMU KWA MPANGO WA MWALIMU MAHIRI (QUALITY EDUCATION THROUGH EXPERT TEACHER SYSTEM (QUEETS). MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anne Mghwira amewataka maafisa Elimu mkoa kwa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanafanya mgawanyo sawa wa walimu katika kila wilaya kwani wilaya za Mwanga na Same zinaupungufu mkubwa wa w...

WAZIRI KAIRUKI AWAFUNDA WANANCHI WANAOCHUKUA MIKOP

Picha
                          SAME.                          WAZIRI WA MADINI ANGELLAH KAIRUKI (WA TATU KUSHOTO) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO CHA WALIMU SAME SACCOS.   WAZIRI wa Madini, Angellah Kairuki amewataka wananchi wanaokopa fedha katika taasisi mbalimbali kuwa makini na kusoma na kuelewa mikataba inayotolewa na taasisi hizo kabla ya kuchukua mkopo ili kuepuka kubebeshwa mzigo mkubwa wa riba. Waziri Kairuki alitoa wito huo mwishoni mwa wiki katika mkutano mkuu wa 19 wa chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Walimu Same Saccos iliyopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Alisema kuwa, zipo baadhi ya taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mikopo kwa wananchi kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi badala yake zimekuwa zikiwakandamiza kupitia mikataba yao hali ambayo hupelekea mkopo kugeuka ...

UVCCM SIHA YAZINDUA KAMPENI YA KUGAWA TAULO ZA KIKE KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Picha
                                                              SIHA MWENYEKITI WA WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI  (UVCCM) WILAYA YA SIHA WILSON MUSHI UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameanza kampeni maalum ya kugawa taulo za kike katika shule za msingi na sekondari wilayani humo yenye lengo la kuhakikisha wananfunzi wa kike waliofikia katika umri wa kuvunja ungo wanashiriki masomo katika kipindi chote wanapofikia katika siku zao za hedhi. Kampeni hiyo iliyozinduliwa jana na Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Siha, Wilson Mushi alisema kuwa, katika utafiti uliofanywa mwaka 2014 wilayani humo kulibainika kuwa asilimia 82 ya wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo pindi wanapokuwa katika si...

MABIHYA AWAKABIDHI SWALA LA ULINZI WA WANANCHI WA KATA YA MAWENZI NA MAKANYA KWA UVCCM

Picha
Mishima. KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KILIMANJARO, JONATHAN MABIHYA WA KATI KATI AKIWA KATIKA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA MKOA WA KILIMANJARO JANA, KUSHOTO NI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA KILIMANJARO, IVAN MOSHI NA KULIA NI KATIBU WA UVCCM MKOA ABDULRAHIMU HAMAD. VIJANA wa chama cha mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kuhakikisha wanalinda wananchi wa kata ya Mawenzi iliyopo manispaa ya Moshi pamoja na Makanya wilayani Same wasitishwe na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani. Alidai kuwa kata hizo mbili zinazotarajia kupiga kura Agosti 12 mwaka huu kumpata Diwani atakayewaongoza kipindi kilichobakia wamekuwa wakitishwa na baadhi ya viongozi wa vyama. Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya katika ufunguzi wa baraza la UVCCM mkoa wa Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, vijana wa chama cha mapinduzi wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi na wanachama wa ccm wanatimiza maamuzi yao ya kikatib...

WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA SIASA CHAFU

Picha
                                                                    MOSHI. MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MAWENZI, MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA KILIMANJARO, DAUDI MRINDOKO (katikati), AKIWA NA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA MAWENZI  CHRISTINE SHIRIMA (kushoto), NA KULIA NI MWENYEKITI WA BODI YA SHULE HIYO PROFESA CHAMBO. WAHITIMU wa kidato cha sita mwaka 2018, nchini wameshauriwa kuacha tabia ya kufanya siasa chafu pamoja na biashara haramu ya madawa ya kulevya na badala yake watumie elimu waliyoipata katika kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, Daudi Mrindoko katika mahafali ya 26 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Mawenzi iliyopo manisp...

UVCCM KILIMANJARO:Maalim Seif Ujiuzulu siasa umechoka

KILIMANJARO. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa Kilimanjaro  umesema siasa za maji taka, uongo fitna na majungu, zimepitwa na wakati hivyo umemtaka Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akubali kiungwana kujiuzulu siasa na kupumzika. Umeeleza kuwa Mwanasiasa huyo hadi leo kubaki kwenye ulingo wa siasa wakati wenzake wengi wameachia ngazi ,yaonyesha ana ajenda ya siri ambayo mtu mwingine ndani ya CUF hana siri hiyo . Matamshi hayo yametamkwa jana na Katibu  wa UVCCM Mkoa Kilimanjaro Abdulrahim Hamid  alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tuhuma dhidi ya Makamo wa Rais Mama Samia zilizotolewa na Maalim Seif hivi karibu wakati akiwa mkoa Kusini Unguja . Hamid alisema kama yupo mwanasiasa mwenye vyama viwili Zanzibar hawezi kuwa mbele ya Maalim Seif kwani ndiye mwanasiasa mwenye vigezo vyote vya kuwa na imani ya kisiasa na kadi mbili kwa wakati mmoja . Alisema si jambo la kawaida kama kweli Maalim Seif si rafiki wa serikali za CCM aweze kuingia kwenye vikao maz...